Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC aingilia kati kuinusuru Stand United

IMG 20230226 WA0011 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Christina Mndeme

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Christina Mndeme ameongoza kikao cha wadau wa michezo wa mkoa wa Shinyanga, kujadili na kutafuta suluhu ya kuikomboa kiuchumi klabu ya Stand United FC inayoshiriki ligi ya Championship Tanzania.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimeazimia kuunda kamati ya watu sita (6), itakayokuwa na jukumu la kuweka mipango mikakati ya kutafuta wadhamini na wadau mbalimbali wa kuisapoti timu hiyo, ili kufikia lengo lake la kucheza ligi kuu.

Pia katika kikao hicho, kiasi Cha shilingi Milioni 8.74 zimechangwa, ambazo kati ya hizo pesa ya mkononi (cash) ni Milioni 1.66, ahadi ni Milioni 7.80, ambazo zimekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kwa niaba ya kamati hiyo iliyoundwa leo.

Aidha Mkuu wa Mkoa Mhe. Mndeme ameipongeza na kuishukuru kampuni ya Jambo Food Products kwa kuisaidia timu hiyo kwa kipindi kirefu, huku akiwataka wadau na makampuni mengine kushirikiana nayo katika kuisaidia Stand United FC.

Stand United FC Kwa sasa inakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha za uendeshaji, kiasi inashindwa kulipa mishahara, kusafiri vizuri, chakula, posho za wachezaji n.k, hivyo kikao hicho wenda kikaleta ahueni katika timu hiyo ambayo inashika nafasi ya 9, ikiwa na alama 19, ikishinda mechi 5, sare 4 na kupoteza 5 kwenye msimo wa ligi ya Championship msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live