Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Homera aingilia kati kuinusuru Mbeya City

Homera.png RC Homera aingilia kati kuinusuru Mbeya City

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema amehuzunishwa na kipigo walichopata Mbeya City kwenye mchezo wa mtoano mkondo wa kwanza kuisaka nafasi ya kucheza ligi kuu Tanzania Bara Msimu ujao kwa kutandikwa na Mashujaa ya Kigoma.

Homera amesema katika kuhakikisha Mbeya City inapata matokeo ya kuibakisha timu hiyo ligi kuu mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Mashujaa ya Kigoma hakutakuwa na kiingilio.

Ikumbukwe katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma hakukuwa pia na kiingilio kwenye mchezo huo ambao Mashujaa waliibuka na Ushindi wa bao 3-1.

Mchezo huo wa Mkondo wa pili utapigwa Juni 22 katika dimba la Sokoine na mshindi wa jumla atajihakikishia ushiriki wa ligi kuu msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live