Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RASMI: Namungo wamvuta Katambi

Namungo Katambi kocha Denis Kitambi ajiunga Namungo

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa klabu ya Namungo, kupitia kwa katibu wake, Omary Kaaya umethibitisha kumuongeza kocha Denis Kitambi kwenye benchi lao la ufundi akiwa kama kocha msaidizi.

Kaaya ameliambia Mwanaspoti, wamemuongeza Kitambi kwenye benchi lao ili lilizidi kuwa pana na kusaidia timu yao ifanye vizuri.

"Kitambi ni kocha wetu msaidizi na tumemuongeza kwa sababu tunajua ana ubora kwenye kuusoma mchezo, atasaidiana na kocha mkuu kwenye kushauriana kwenye benchi la ufundi," amesema Kaaya.

Kaaya alipoulizwa kuhusu mkataba walioingia na kocha huyo amesema;"Siwezi kusema tumesaini nae mkataba wa muda gani ila elewa ni kocha wetu."

Kitambi anasifika na soka maridadi la chini pindi anapokuwa anafundisha timu yoyote ile.

Kocha huyo aliwahi kuifundisha AFC leopards ya nchini Kenya na baada ya Simba kuvutiwa na huduma yake ilimrejesha nchini na kurithi nafasi ya Masoud Djuma ambaye aliondolewa.

Kitambi alipita pia katika kikosi cha Azam akiwa kama kocha msaidizi na msimu uliopita alikuwa kwenye kikosi cha fountain Gate kinachoshiriki Ligi ya Championship.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live