Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RASMI: Eritrea yajiondoa kufuzu Kombe la Dunia 2026

Eritrea1 Timu ya Taifa ya Eritrea

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CAF na FIFA wamethibitisha kujiondoa kwa Eritrea kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia 2026,

Eritrea ambayo ilipangwa kundi E ilitakiwa icheze mchezo wake wa kwanza dhidi ya Morocco mapema mwezi huu.

Kwa mujibu wa Guardians sports wanadai kuwa chanzo cha Eritrea kujiondoa ni kuhofia kuwapoteza baadhi ya nyota wake ambao wamekuwa na tabia ya kuzamia kwemye mataifa ambayo wamekuwa wakienda kucheza michezo yao mbalimbali na timu yao ya taifa.

Mabingwa hao wa CECAFA challenge 2019 walikumbwa na kadhia ya nyota wake kuzamia mataifa ambayo wamekuwa wakienda kucheza kuhofia usalama wao wakati huu ambao nchi iko chini ya utawala wa kijeshi chini ya Rais Isaias Afwerki.

Tangu 2009 Inakadiriwa wachezaji wapatao 60 wameomba hifadhi maalumu kwenye mataifa mbalimbali kwa kutumia ngao ya uanamichezo kupata hifadhi hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live