Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RASMI: Chelsea wamalizana na Lampard

Lampard 1 Frank Lampard

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumteua aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Frank Lampard kuwa kocha wa muda/mpito kwa mkataba mpaka mwisho wa msimu huu na kuchukua mikoba ya Graham Potter aliyefutwa kazi.

Lampard (44) raia wa England aliyemewahi kuichezea Chelsea na kuiongoza kushinda ligi ya Mabingwa Ulaya mnamo 2012 kama nahodha amekubali kuchukua nafasi hiyo huku The Blues wakiendelea na mchakato wa kusaka kocha mkuu mpya wa muda mrefu.

Lampard anatarajiwa kuungana na mlinzi wa zamani wa Arsenal na Chelsea Ashley Cole kama kocha wake msaidizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live