Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RASMI: Arne Slot akabidhiwa mikoba ya Klopp Liverpool

Skysports Premier League Liverpool 6533814 Arne Slot akabidhiwa mikoba Liverpool

Tue, 21 May 2024 Chanzo: dar24

Klabu ya Liverpool imemtangaza rasmi aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Feyenoord ya nchini Uholanzi Arne Slot, kuwa mrithi wa Jurgen Klopp aliyeondoka klabuni hapo juzi Jumapili (Mei 19).

Slot alitarajiwa kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la Liverpool kabla ya kutangazwa na Uongozi wa Klabu hiyo, kwani aliwahi kuwathibitishia Waandishi wa Habari nchini kwao kuwa atafanya kazi Anfield kuanzia msimu ujao.

Slot ataanza kazi kama Kocha Mkuu wa The Reds Juni Mosi, akitarajiwa kuendeleza mazuri yaliyoachwa na Klopp ambaye alikuwa na mafanikio makubwa tangu alipotua klabuni hapo mwaka 2015.

Kabla ya kutangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Liverpool, Slot alitoa neno la shukurani kwa Mashabiki wa Feyenoord akisema: “Hakika si uamuzi rahisi kufunga mlango nyuma yako katika klabu ambayo umepitia matukio mengi ya ajabu na kufanya kazi kwa mafanikio kwa kushirikiana na watu wengi.”

“Lakini kama mwanamichezo, nimeipokea kwa moyo mkunjufu nafasi ya kuwa sehemu ya makocha wa Ligi ya England, na katika moja ya klabu kubwa duniani, ilikuwa vigumu kwangu kuikataa fursa hii.”

Klopp alitangaza mwezi Januari kwamba ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kuchoshwa na mahitaji ya moja ya klabu kubwa katika soka la Ulaya.

Kabla ya kutangazwa kwa Slot, wamiliki wa klabu hiyo walikuwa wakihusishwa na makocha kadhaa, akiwemo meneja wa Bayer Leverkusen na kiungo wa zamani wa Liverpool, Xabi Alonso, lakini alichagua kubaki na mabingwa hao wa Bundesliga.

Klopp alijiunga na Liverpool Oktoba 2015 na kushinda Kombe la Ligi mara mbili, Kombe la FA, Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na Ligi ya England mara moja.

Chanzo: dar24