Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Qatar yaongeza meli kukabiliana na uhaba wa hoteli

Cruise Ship Body 3 Render Qatar yaongeza meli kukabiliana na uhaba wa hoteli

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi ya Qatar imeongeza meli nyingine ya kukodi ili kukabiliana na uhaba wa hoteli kwa wageni wanaotarajiwa kwenda kutazama Kombe la Dunia mwezi ujao ambapo hii inakuwa meli ya tatu kupelekwa kwenye taifa hilo.

Meli inaitwa MSC Cruises na inatokea Geneva Uswizi ikiwa na vyumba vya kulala zaidi ya elfu moja ndani yake na itakuwa nchini Qatar kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 19 ambapo bei ya chini ya kulala Mtu mmoja kwa usiku mmoja ni dola 470 (TSH. 1,096,040).

Qatar haina hoteli za kutosha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Timu zote za mpira, Wafanyakazi, Wafanyakazi wa kujitolea na Mashabiki katika Kombe la Dunia ambapo imeamua kuunda maeneo yenye kambi na vyumba, kukodisha meli za kitalii na hata kuwahimiza Mashabiki kukaa katika nchi jirani na kurudi Qatar kwaajili ya mechi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live