Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Qatar 2022: Bia zaruhusiwa kwenye Mashindano ya Kombe la Dunia

Bia Qatar Matumizi ya vileo yameruhusiwa katika mashindano ya Kombela Dunia

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za dunia ambao watasafiri kwenda nchini Qatar wa ajili ya kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia mwaka huu wataruhusiwa kunywa bia kwenye maeneo ya mashabiki na viwanja vyote.

Sera hiyo ya kuruhusu unywaji bia imepitishwa na muandazi wa Mashindano hayo ambapo asilimia kubwa ya wakazi wa nchini Qatar ni waislam, hivyo mashabiki wataruhusiwa kunywa bia kabla na baada ya mchezo kumalizika ndani ya viwanja nane.

Watoa huduma waliruhisiwa kununua champagnes, wine, bia na vileo vikali kama sehemu ya ‘corporate packages’ tangu mwaka 2021.

Kampuni ya AB InBev ambao ni wazalishaji wa bia aina ya Budweiser ndio bia rasmi kwa ajili ya Mashindano ya kombe la Dunia tangu mwaka 1986 na mpaka mwaka huu ndio bia rasmi ya ya msahindano hayo.

Kulingana na FIFA: “Pombe zitauzwa ndani ya viunga vya uwanja kabla ya mechi kuanza na baada ya mechi kuisha”

“Ndani ya uwanja wenye tiketi na vikombe wataweza kupata bia isiyo na kilevi ya Budweiser Zero,” FIFA walisema kwenye waraka huo.

Pia matumizi ya vileo kwenye maeneo ya wazi yamepigwa marufuku, japokuwa hoteli na bar zote zimepewa vibali vya kuuza vileo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live