Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Professor: Nimepokea Jumbe nyingi sana za wenye matatizo ya Figo

Profesa Jay Jizo Msanii wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘Prof Jay’

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘Prof Jay’, amesema amepokea DM nyingi za watu wenye matatizo ya figo muda mfupi baada ya kutangaza kuanzisha foundation yake itakayosaidia wagonjwa wa figo iliyozinduliwa usiku wa kuamkia leo Pamoja na EP yake iliyoitwa ‘Nusu Peponi nusu Kuzimu’ Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Prof Jay ambaye amekuja na foundation hiyo inayotarajiwa kusaidia wagonjwa wa figo amesema ameguswa kutokana na kusumbuliwa na tatizo la figo kwa miaka miwili akitumia gharama kubwa kupata matibabu ameona atumie nafasi hiyo kuwasaidia wengine.

Hadi sasa tumesajili wagonjwa zaidi ya 518 wenye matatizo ya figo ambao wanahitaji kupata msaada kupitia foundation ya Profesa Jay Foundation wakiwa na mahitaji tofauti tofauti.

“Natoa shukrani zangu kwa watu wote waliojitokeza kuniunga mkono na kusaidia wagonjwa mbalimbali wanaopata shida ya figo.”

“Tulifikiria kuanza na kuchangisha lengo letu lilikuwa kiasi cha Sh milioni 800, lengo ni nikuanza na wagonjwa 50, mpaka sasa DM yetu ya Instagram kuna Watu zaidi ya 600 wanaomba msaada kwamba wana hali mbaya, wanategemea Prof Jay foundation iwe kama mwokozi wao”

“Mungu aliingia ndani yangu, mengi yalisemwa sana wakati naumwa, nilitobolewa koo na moyo wangu ulisimama mara tatu, Mungu amesikia kilio cha Watanzania na maombi ya Watanzania, nimecheki vocal cord na inaonesha kabisa haijaguswa, sauti inaendelea kuimarika na itarudi kama zamani, leo nitatoa EP kama zawadi pia kama shukrani yangu kwa Mungu, inatwa Nusu Peponi Nusu Kuzimu ina nyimbo nne” amesema Jay

Chanzo: www.tanzaniaweb.live