Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amezitaka klabu za Yanga, Simba, Azam na Coastal Union ambazo zinaiwakilisha nchi kimataifa, kuwekeza zaidi katika suala la kupima afya za wachezaji wanaowasajili kwa kuangalia hususanmaeneo makuu mawili ambayo ni utimamu wa afya ya magoti na moyo.
“Hizi klabu zinatumia fedha nyingi sana kusajili wachezaji hao wa kigeni, kabla ya kuwapa mkataba wanalazimika kuwapima afya zao, Mlonganzila tupo tayari kuangalia afya za wachezaji hao wanaowasajili."
“Mfano upo hivi karibuni tumeona moja ya klabu haikuweza kumtumia mchezaji wake aliyesajiliwa kwa gharama kubwa na kucheza mechi moja au mbili na kukosa msimu mzima,” amesema Profesa huyo.
Pia amewataka viongozi wa vilabu hivyo kutodangayika na ‘Clip’ za YouTube wanazotumiwa kuangalia wachezaji kwa ajili ya kuwasajili na kuhakikisha wanawapima afya.