Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Privadinho: Hii ni chachu kwa vijana wa kitanzania

Priva.png Priva Abiudi Shayo

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: dar24.com

Msimamizi wa Maudhui ya Mitandaoni (Digital Manager) ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Priva Abiudi Shayo amesema nafasi aliyoipata ndani ya klabu hiyo naitazama kama chachu ya kuwahamasisha vijana wa kitanzania kuaminiwa katika taasisi kubwa.

Pviva ‘Privadinho’ alitangazwa kushika nafasi hiyo jana Jumanne (Septemba 27) sambamba na mwenzake Ally Kamwe ambaye anakuwa Afisa Habari wa Young Africans, akirithi nafasi ya Hassan Bumbuli.

Amesema: “Nafasi niliyoipata Young Africans siingalii zaidi kwa upande wangu ila naiangalia kama chachu na hamasa kwa vijana”

“Mimi bado ni kijana mdogo lakini tazama historia na ukubwa klabu ya Young Africans. Ni klabu kubwa si tu Tanzania bali hata nje ya mipaka ya Tanzania.”

“Taasisi kubwa kama Young Africans imeonesha imani vijana wadogo, basi ni hamasa kubwa kwa vijana ambao wanakuja kwenye tasnia iwe ni Waandishi au Wachambuzi, tayari kuna mwanga umeanza kuonekana.”

Chanzo: dar24.com