Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons yapata ushindi baada ya siku 52

Dodoma Live Prisons yapata ushindi baada ya siku 52

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kusota kwa siku 52 bila ushindi, hatimaye leo Tanzania Prisons imefufuka na kupata pointi tatu kwa kuichapa Dodoma Jiji bao 1-0.

Prisons mara ya mwisho kushinda ilikuwa Oktoba 8 ilipoitandika Mtibwa Sugar mabao 3-2 na kufanya presha kuwa kubwa kwa viongozi na mashabiki wa timu hiyo hadi kufikia uamuzi wa kutimua aliyekuwa kocha mkuu, Fred Felix 'Minziro'.

Leo ikicheza kwa ubora na utulivu chini ya kocha mpya, Ahmad Ally, Maafande hao walisubiri hadi dakika ya 78 walipoandika bao kupitia kwa Nahodha wao, Jumanne Elfadhir kwa penalti baada ya Edwine Balua kuangushwa eneo la hatari na Adeyun Saleh.

Hata hivyo Dodoma Jiji licha ya kuupiga mwingi ilijikuta ikibaki pungufu kufuatia beki wake wa kati, Joram Mgeveke kumchezea rafu Edwin Balua wa Prisons na kuoneshwa kadi nyekundu na kuwafanya wenyeji kuonekana kutakata zaidi.

Kabla ya bao hilo Prisons ilikosa mabao ambayo yangewapa wastani mzuri ikiwamo la dakika ya 73 mpira wa faulo baada ya Balua kuangushwa na Mgeveke ambao shuti lake lilitoka nje ya lango, huku Dodoma nao wakikosa nafasi kadhaa.

Huo unakuwa ushindi wa pili kwa Wajelajela kati ya mechi 12 walizocheza na kufikisha pointi 10 huku Dodoma Jiji ikipoteza mechi ya pili mfululizo baada ya ile dhidi ya Singida Fountain Gate walipokufa nyumbani 2-1.

Kufuatia ushindi huo, mastaa wa Prisons wataoga minoti kutoka kwa wadhamini wao Bens Agro Star ambao walitangaza dau la Sh1 milioni kwa kila bao la ushindi, huku Kocha mkuu akiweka kibindoni Sh 500,000.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: