Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons yaiandalia sapraizi Simba

Prisons FC Prisons yaiandalia sapraizi Simba

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mkuu wa timu ya Tanzania Prisons, Hamad Ally amesema wanaandaa sapraizi kwa ajili ya mchezo wao na Simba huku akisisitiza wataingia kwa tahadhari kubwa wakiwaheshimu wapinzani wao kwa kuwa wamekuwa na ubora kwenye michezo yao.

Hamad amesema Simba wamekuwa na kiwango bora kwenye michezo yao ya siku za hivi karibuni, hivyo wamejipanga kuingia na kitu ambacho kitawawezesha kupata matokeo mbele yao.

"Kiuhalisia Simba inao wachezaji wazuri ambao kama ukifanya makosa ya kujirudia rudia watakuadhibu, kwa kulifahamu hilo tumejiandaa kuwaheshimu na kucheza kaa tahadhari kubwa ili tuweze kupata kile tunachokihitaji.

"Tumewafuatilia Simba kwa michezo yao ya siku za hivi karibuni kupitia mikanda ya video na tumebaini udhaifu wao, hivyo tunajua nini tutakachokifanya ili tuweze kupata matokeo yatakayoendelea kutuweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo."

Ally ambaye ameiongoza Prisons katika michezo 7 ya ligi na kupoteza mchezo mmoja, akitoa sare mbili na kushinda nne, amesema hawatakubali kuwa wanyonge kwenye mechi yao na Simba.

"Iko wazi kwamba Simba amekuwa na bahati ya kupata matokeo mbele ya Prisons lakini kwa mechi ya kesho itakuwa tofauti maana tumejipanga kivingine, na katika wiki hii tumekuwa na maandalizi tofauti ambayo yatatufanya tuondoe uteja lakini nasisitiza lazima tuwaheshimu Simba."

Simba inaenda katika mchezo huo ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya michezo 15 ambapo imekusanya alama 36 ambapo Simba itatakiwa kushinda ili kujikita kwenye nafasi za juu katika msimamo ambao wanazidiwa na Yanga alama saba huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi. Azam iko nafasi ya pili kwa pointi 43 pia, lakini imezidiwa tofauti ya mabao na Yanga, lakini Wanalambalamba wamecheza mechi nne zaidi ya Simba.

Prisons wako nafasi ya sita kwenye msimamo baada ya michezo 18 ambapo wamekusanya jumla ya alama 24 na wako na wakati bora tangu Novemba 23 mwaka jana walipompata kocha Hamad Ally aliyeifanya timu icheze soka zuri la matokeo chanya.

Chanzo: Mwanaspoti