Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons yafuta uteja kwa Geita Gold, yaitungua 3-1

TANZANIA PRISONS.png Prisons yafuta uteja kwa Geita Gold, yaitungua 3-1

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania Prisons imeandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika uwanja wa Nyankumbu mjini Geita baada ya kuifumua Geita Gold mabao 3-1 na kufuta uteja dhidi ya wapinzani hao.

Geita Gold haijawahi kupoteza mchezo wowote kwenye uwanja wake huo tangu ikiwa Championship na jana Aprili 24 haijaamini kilichowatokea baada ya kulizwa kwa kipigo hicho.

Mabao katika mchezo huo yamefungwa na Jeremia Juma dakika ya tatu, Samson Mbangula dakika dakika ya 68 na Edwine Balua dakika ya 77 na kufikisha pointi 31 na kupanda nafasi ya tisa kwenye msimamo, huku la Geita likifungwa na Juma Liuzio.

Hizi ni dondoo fupi za mechi hiyo.

Tanzania Prisons inakuwa ushindi wake wa tatu mfululizo chini ya Kocha wake Abdalah Mohamed 'Baresi' ikianza dhidi ya Namungo ugenini 3-2, kisha ikaichapa Ruvu Shooting 3-1 na leo inatakata mbele ya matajiri hao wa mjini Geita.

Kama haitoshi Wajelajela hao wanafuta uteja dhidi ya wapinzani hao kwani katika mechi tatu walizokuwa wamekutana ligi kuu, walipata sare moja na kupoteza miwili ikiwamo kipigo cha 4-1 katika msimu uliopita walipokutana uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Straika Jeremiah anafikisha mabao tisa kwenye ligi kuu na kuendelea kuongoza kwenye kikosi hicho na kuwafikia John Bocco (Simba), Sixtus Sabilo (Mbeya City) Bruno Gomes (Singida BS) na kuwapumulia Moses Phiri na Saidoo Ntibazonkiza (Simba) wenye mabao 10 kila mmoja.

Pamoja na kupoteza mchezo huo, Geita Gold inabaki nafasi yake ya tano kwa pointi 37 ambapo timu zote zimebakiza mechi tatu kumaliza msimu huu.

Leo ilikuwa mchezo wa nane kwa kocha ‘Baresi’ tangu ajiunge na Maafande hao ambapo amepoteza mechi tatu dhidi ya Yanga kombe la shirikisho (4-1) akafungwa 1-0 na Coastal Union sawa na Polisi Tanzania, sare moja dhidi ya Mtibwa Sugar na kushinda mitatu kama ilivyotajwa huko juu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: