Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons yafufuka, Mtibwa hali tete

Prisons Vs Mtibwa Nn Prisons yafufuka, Mtibwa hali tete

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kucheza mechi nne mfululizo bila kuonja ushindi hatimaye Tanzania Prisons imefufuka leo kwa kuikanda Mtibwa Sugar mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu.

Matokeo hayo yanaifanya Prisons kujinasua mkiani na kupanda nafasi ya 14 kwa pointi nne huku Mtibwa wakishuka hadi nafasi ya 15 kwa pointi mbili baada ya mechi tano kila timu.

Katika mchezo huo ambao umepigwa uwanja wa Sokoine jijini hapa, Mtibwa ndio walitangulia kupata mabao kupitia kwa Matheo Anthony na Abal Kassim, huku Edwine Balua, Benno Ngassa na Joshua Nyatin wakiifungia Prisons.

Kabla ya mchezo huo, Prisons ilikuwa imepata sare moja dhidi ya Singida Fountain Gate na kupoteza mitatu dhidi ya Azam 3-1, Tabora United 3-1 na kufa kwa Simba 3-1.

Huu unakuwa ushindi wa kwanza kwa kocha mkuu, Fred Felix 'Minziro' tangu ajiunge na timu hiyo mapema msimu huu baada ya kuaminiwa na Wajelajela hao.

Mtibwa Sugar inafikisha mchezo wa tano bila kuonja ushindi ikiwa ni sare mbili chini ya kocha wake, Habibu Kondo na kuwa nafasi ya 15 kwa pointi mbili katika Ligi Kuu.

Winga wa Prisons anafikisha mechi mbili mfululizo akifunga bao na kufikisha mawili katika akaunti yake huku Anthony wa Mtibwa Sugar akifiksha mabao matatu katika Ligi Kuu.

Prisons inaweka rekodi ya kipekee kwa Mtibwa Sugar kwani katika michezo mitano waliyokutana ikiwamo wa leo unakuwa ushindi wa pili sare mbili na kupoteza mmoja.

Pamoja na matokeo hayo, timu hizo zinakuwa na mwendelezo wa kuruhusu mabao, ambapo Prisons imeruhusu 11 hadi sasa ikifunga manne tu, huku Mtibwa wakiruhusu tisa na kufunga manne.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: