Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons yaanza kujiwinda na Polisi Tanzania

Proizon Pic Data Prisons yaanza kujiwinda na Polisi Tanzania

Thu, 21 Apr 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baada ya mapumziko mafupi leo Tanzania Prisons imeanza mazoezi kujiandaa na mwendelezo wa Ligi Kuu, hasa mchezo wake ujao dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Mei Mosi jijini hapa.

Timu hiyo ilikuwa na mapumziko mafupi ya takribani siku nne tangu ilipomaliza mechi yake na Coastal Union, Aprili 18 na kushinda bao 1-0.

Leo Alhamisi kikosi hicho kimeanza kujifua, ambapo licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake na Kocha Mkuu, lakini hakikuharibika kitu chini ya msaidizi, Shaban Mtupa na Meneja, Osward Moris.

Wajelajela hao ambao kwa sasa wanapambana kujinasua nafasi za mkiani, walitumia zaidi ya saa mbili kujinoa ambapo Kocha Mtupa alielekeza zaidi macho yake kwenye fiziki, kumiliki mpira, pumzi na kuhitimisha na kufunga mabao.

Wachezaji ambao hawakuonekana katika matizi hayo, ni Nahodha, Benjamin Asukile ambaye imeelezwa ana ruhusa maalumu ya kifamilia na kesho anatarajia kuwapo kwenye mwendelezo wa maozezi.

Wengine ni Straika, Samson Mbangula ambaye anasubiri kofia maalumu baada ya kuumia mwezi uliopita, Salum Kimenya ambaye bado hajarejea uwanjani na Jumanne Elfadhiri ambaye yupo nchini Kenya kwa uchunguzi wa afya yake.

Pia Jeremiah Juma na Ezekiel Mwashilindi nao imeelezwa hawako fiti kiafya lakini matarajio yao ni kufikia Jumatatu ya wiki ijayo kurejea kwa maandalizi rasmi ya mchezo dhidi ya Maafande hao.

Kwa upande wa Kocha Mkuu, Odhiambo imeelezwa kuwa yupo kwao nchini Kenya kwa mapumziko mafupi na kufikia Jumatatu ijayo anatarajia kuwa amerejea kuendelea na majukumu yake.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Jackson Mwafulango amesema pamoja na mapungufu hayo, lakini si kwamba itapunguza chochote kwenye mipango yao isipokuwa mikakati iko palepale kuhakikisha Prisons inafanya viziuri.

"Leo tumeanza mazoezi kujiandaa na Polisi Tanzania, hawa ambao hawapo kila mmoja ana sababu zake ambazo zinafahamika lakini kufikia Jumatatu ijayo tutakuwa kamili tayari kwa maandalizi ya mchezo ujao na tunaamini alama tatu tutabaki nazo Sokoine" amesema Mwafulango.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz