Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons yaangukia neema nyingine

Prison Mkataba Prisons yaangukia neema nyingine

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Tanzania Prisons imeendelea kula shavu baada ya leo kuingia mkataba wa takribani mwaka mmoja na kampuni ya Jordan Pure drinki Water ya jijini Mbeya ikiwa ni udhamini wa pili kwa timu hiyo ya Ligi Kuu msimu huu.

Mkataba huo umesainiwa leo Novemba 18 katika ofisi za kampuni hiyo kwa kushirikisha Katibu Mkuu wa Tanzania Prisons, Anthony Hau na Meneja wa kampuni, Hyasinta Tarimo.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo wa miezi nane, Hau ameishukuru kampuni hiyo kujiunga na familia ya michezo hususani Tanzania Prisons na kwamba anaamini udhamini huo utasaidia katika uendeshaji wa klabu.

Amesema timu ya vijana (U20) na ile ya wakubwa zote zitakuwa zikitumia maji ya kampuni hiyo popote huku akieleza kuwa klabu itatekeleza makubaliano yote kwa mujibu wa mkataba.

“Kwanza niishukuru kampuni hii kwa kujiunga na familia ya Tanzania Prisons, tutahakikisha tunatekeleza matakwa ya kimkataba hasa timu za vijana na ile ya wakubwa tunatumia maji haya,” amesema Hau.

Kwa upande wake Meneja Hyasinta amesema kampuni itakuwa inatoa katoni 120 kwa mwezi, huku akibainisha kuwa mkataba unaweza kuboreshwa mwakani iwapo timu itabaki ligi kuu.

“Sisi kampuni tumeona fahari kushirikiana na Tanzania Prisons, tunaweza kuboresha mkataba kutegemea na mafanikio na zaidi timu kubaki ligi kuu, tumeanza na timu hiyo kwakuwa ni ya nyumbani na baadaye ttazifikia nyingine,” amesema hyasinta.

Chanzo: Mwanaspoti