Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons kurekebisha makosa yao

9d2c37f69f7424a10418d9288345447a.jpeg Shaban Kazumba

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Timu ya Tanzania Prisons imepania kurudisha kiwango chake katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuanza msimu vibaya.

Akizungumza kocha msaidizi wa Prisons, Shaban Kazumba amesema hawakuwa na mwanzo mzuri wa ligi na hicho kilichowakuta anaamini ni upepo ambao utapita.

Tanzania Prisons katika michezo mitano iliyocheza haijashinda hata mmoja zaidi ya sare mbili na kupoteza michezo mitatu.

“Matokeo ya mechi zetu zilizopita hayakuwa mazuri nadhani ni upepo tu, bado tuna matumaini tutarudi katika kasi yetu kama wa- chezaji watatuliza akili na kupambana kupata ushindi,” alisema.

Kazumba amesema amewaeleza wachezaji umuhimu wa michezo ijayo ambapo wanatarajiwa kuwakaribisha Mbeya Kwanza Novemba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Amesema kulingana na mambo yalivyo, wakishinda mchezo mmoja wanaweza kutoka chini na kupanda nafasi za juu hivyo hawana wasiwasi.

Kocha huyo alisema mchezo huo ujao una umuhimu na wanajua Mbeya Kwanza siyo timu ya kubeza kwani imeanza ligi vizuri hivyo wataingia kucheza kwa kujiamini lakini kwa tahadhari wakijua pointi tatu zinahitajika.

“Mbeya Kwanza tulicheza nao mchezo wa kirafiki tukawafunga lakini hatuwabezi, hatuwezi kujua watakuja vipi, ni lazima tuwaheshimu,” amesema.

Prisons inaonekana kuwa na safu mbovu ya ulinzi na ushambuliaji wakifungwa jumla ya mabao sita na ku- funga bao moja pekee katika michezo mitano.

Timu hiyo inashika nafasi ya pili kutoka mwisho ikiwa na pointi mbili huku walioko mwisho ni KMC wanaofanana kwa kila kitu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz