Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons kuivaa KMC, Shooting vs Ihefu

89163f5a7322f71e939d73e85a876ed5.jpeg Prisons kuivaa KMC, Shooting vs Ihefu

Fri, 12 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

LIGI Kuu Tanzania Bara mzunguko wa 19 utaendelea leo kwa michezo miwili kuchezwa katika viwanja vya miji tofauti.

Tanzania Prisons itacheza na KMC katika Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa na Ruvu Shooting watawakaribisha Ihefu FC kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani,

Mchezo wa Prisons na KMC unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kwani KMC itahitaji kuendeleza ushindi baada ya kutoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC mechi iliyopita, wakati Tanzania Prisons ilitoka sare 1-1 na Yanga.

KMC inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza michezo 18, huku Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo ikiwa na pointi 22.

Rekodi za msimu uliopita walipokutana Septemba 12, 2020 zinaonesha KMC iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha msaidizi wa KMC, Habibu Kondo alisema utakuwa na ushindani kwa kuwa wanakwenda kukutana na wapinzani ambao ni wagumu kupoteza mchezo wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani.

“Mchezo utakuwa na ushindani kwa kuwa tunakwenda kucheza na kikosi ambacho kinacheza soka la kujilinda muda mwingi lakini pia ni wagumu kupoteza wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu,” alisema.

Kondo alisema wanahitaji matokeo mazuri kwani baada ya kushinda mchezo uliopita morali ni kubwa na benchi la ufundi limetimiza majukumu lao la kuwapa mbinu wachezaji watakazotumia kwenye mchezo huo.

Ruvu Shooting inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 28 na Ihefu iliyopo mkiani ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza michezo 18.

Chanzo: habarileo.co.tz