Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons hali tete ikiisubiri Yanga

Prisons Hali Tete Prisons hali tete ikiisubiri Yanga

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Matokeo mabovu inayoendelea kuvuna Tanzania Prisons kwenye Ligi Kuu inazidi kuwaweka kwenye hatari ya kukaa nafasi za kushuka daraja.

Katika michezo 14 iliyocheza imeshinda michezo mitatu, sare sita na kufungwa michezo mitano na kuifnya Prisons kuwa na alama 15 alama tatu nyuma ya Ruvu Shooting ambayo ipo nafasi ya kucheza hatua ya mtoano.

Mara ya mwisho Prisons kupata ushindi ilikuwa Oktoba 25 Uwanja wa Sokoine ilipoichapa Polisi Tanzania mabao 2-1 yaliyofungwa na Jeremiah Juma pamoja na Samson Mbangula, michezo mingine ambayo Prisons imeshinda ni ile dhidi ya Dodoma iliposhinda 2-1, dhidi ya Azam FC (1-0).

Kocha timu hiyo, Patrick Odhiambo alisema matokeo sio mazuri kwao na wanaendelea kujitahidi kuhakikisha wanakuwa na matokeo mazuri katika michezo ijayo.

“Hakuna anayefurahia matokeo haya sababu sio mazuri kwetu na hata mashabiki wetu. Kikubwa kama benchi la ufundi tunaendelea kurekebisha makosa kila baada ya mchezo,” alisema Odhiambo.

Hata hivyo, mshambuliaji wa timu hiyo, Jeremiah Juma alisema bado timu inatafuta morali kutokana na matokeo mabaya ambayo wamekuwa wakiyapata, lakini alama moja waliyoipata dhidi ya KMC kwao ni kama ushindi.

“Hali sio nzuri kwetu kwa kuwa michezo mitatu tumefungwa lakini kupata alama tatu ugenini ni kama ushindi hivyo tunajitahidi ili kurudi katika hali ile tuliyokuwa tumeanza nayo ligi,” alisema Juma.

Tanzania Prisons sasa inajiandaa kuikabili Yanga ambayo jana ilikuwa Uwanja wa Highland Estates, Mbarali kuikabili Ihefu na kabla ya hapo iliifunga Mbeya City 2-0 Uwanja wa Mkapa.

Msimu uliopita Tanzania Prisons iliponea tundu la sindano kushuka baada ya kuishia hatua ya mtoano kwa kucheza na Mtibwa Sugar ambayo nayo ilikutana na JKT Tanzania hatua ya mwisho na kupata ushindi ulioibakisha Ligi Kuu.

Chanzo: Mwanaspoti