Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons hali tete Sokoine

Play Offs.jpeg Prisons hali tete Sokoine

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu ya Tanzania Prisons imeshindwa kutumia vyema Uwanja wake wa Sokoine baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa kwanza wa mtoano (Play-Off) kutafuta tiketi ya kusalia Ligi Kuu Bara.

Shujaa wa Mtibwa Sugar alikuwa ni Jaffar Kibaya aliyefunga mabao mawili dakika ya 22 na 55 huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Salum Kanoni dakika ya 71.

Kwa upande wa Prisons ilijipatia bao la kufutia machozi kunako dakika ya 59, kupitia kwa Marco Mhilu aliyeingia kipindi cha pili.

Mchezo huo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku zikishambuliana kutafuta matokeo mazuri ili kujiweka fiti kabla ya kurejeana.

Timu hizi zimekutana hatua hii baada ya Prisons kumaliza ya 14 huku Mtibwa Sugar ikimaliza nafasi ya 13.

Mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu Bara msimu ujao na atakayefungwa ataendelea kucheza 'Play'Off' dhidi ya JKT Tanzania.

Matokeo haya yanakuwa na faida zaidi kwa Mtibwa Sugar kabla ya kurejea tena Julai 6, kwenye Uwanja wa Manungu Morogoro.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz