Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons chupuchupu, Kichuya acheka na nyavu

Namungo Vs Prisons Kichuya Prisons chupuchupu, Kichuya acheka na nyavu

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao la kujifunga kwa beki wa Namungo, Frank Magingi limeifanya timu hiyo kuondoka na alama moja dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa leo Jumamosi katika uwanja wa Sokoine jijini hapa.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkali ambapo kila timu ilihitaji alama tatu ili kujiweka pazuri, ambapo Prisons iliingia uwanjani ikijivunia rekodi ya ushindi wa mabao 3-1 walipokutana msimu uliopita katika uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Kipindi cha kwanza timu zote zilionekana kuchangamka na kushambuliana, japokuwa Namungo ndio walikuwa bora kutokana na mipira yao kuwa na macho na kuwasumbua mabeki wa Prisons wakiongozwa na Nahodha Msaidizi, Jumanne Elfadhir.

Hata hivyo Namungo haikuwachukua muda mrefu, kwani dakika ya 21, Winga wake machachari aliweza kuwatanguliza kwa bao la kwanza baada ya kupokea pasi kutoka kwa Frank Magingi na kutembea nao hadi alipoaamua kukunjuka shuti na kujaa wavuni.

Wajelajela walijaribu kupambana kulazimisha mashambulizi, ambapo Kipa wa Namungo, Jonathan Nahimana alikuwa imara sambamba na mabeki wake kuweka lango salama na kufanya dakika 45 za kwanza zikimalizika wakiwa mbele.

Dakika ya 51 na 56 Namungo waliwatoa Ally Kiyembe na Mohamed Issa kuwapisha Reliant Lusajo naKassim Shaban, huku Priosns wakiwatoa Samson Mbangula na Omary Omary na kuwaingiza Ismail Mgunda na Marco Mhilu.

Pia Maafande hao waliwapumzisha Jeremiah Juma na Michael Ismail na kuingia Benjamin Asukile na Zabona Hamis katika dakika ya 70, mabadiliko ambayo yaliipa faida timu hiyo kuisawazisha dakika ya 90 kupitia kwa Magingi aliyejifunga wakati akiokoa hatari langoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live