Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons: Simba kitu gani bwana!

TZ Prisons Winner Kikosi cha Tanzania Prisons

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Matokeo ya ushindi katika mechi mbili mfululizo, yameonyesha kuwapa mzuka Tanzania Prisons wakitamba kuwanyoosha Simba watakapokutana kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Licha ya Simba kujivunia ushindi wa 1-0 katika mechi ya raundi ya kwanza baina yao kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, lakini katika michezo miwili nyuma dhidi ya wapinzani tofauti wa Ligi Kuu, Mbeya City imekusanya alama sita wakati Simba imekusanya alama nne.

Prisons imeshinda mechi zake mbili ikiwa nyumbani ikianza dhidi ya Dodoma Jiji 2-0 na Mbeya City 2-1 huku Simba ikishinda mmoja kwa KMC 3-1 na sare ya 1-1 na Kagera Sugar zote ikicheza ugenini.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Patrick Odhiambo, alisema vijana wako fiti na morali iko juu wakichagizwa na matokeo ya mechi mbili mfululizo waliyopata hivyo kwa Simba pia wanatarajia alama tatu.

Alisema wanafahamu ugumu wa Simba haswa inapokuwa kwenye Uwanja wa Taifa, lakini wataingia na mbinu kuwabana wachezaji wenye madhara ili kufikia malengo.

“Kucheza na Simba inahitaji utulivu kwa sababu wanao wachezaji wenye uwezo binafsi lazima tuangalie mmoja mmoja na kujua namna ya kumdhibiti” alisema Odhiambo.

Nahodha wa timu hiyo, Benjamin Asukile alisema hawana hofu yeyote katika mechi hiyo na wanaenda kupambana kuwania alama tatu ambazo zitawaweka pazuri katika msimamo.

Alisema mara kadhaa wanapokutana na Simba mechi huwa na upinzani mkali lakini watakuwa makini kutoruhusu mashambulizi yanayoweza kuwagharimu.

“Sisi tuko vizuri kisaikolojia na kiushindani, kila mmoja ana ari kuhakikisha mchezo huo tunaondoka japo na pointi yoyote, Simba anafungika ni kujiamini tu,” alisema mkongwe huyo.

Chanzo: Mwanaspoti