Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons: Mayele hapiti, wachekelea rekodi

IMG 4255.jpeg Wachezaji wa Yanga

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Yanga wakitambia nyota wake Fiston Mayele kufunga mabao kesho dhidi ya Tanzania Prisons ili kutwaa tuzo ya mfungaji bora, Wajelajela wamesema wako fiti na hawatarajii kupoteza mchezo huo na straika Mayele hatafurukuta huku wakichekelea rekodi yao.

Tangu Mayele atue nchini misimu miwili sasa, hajawahi kuifunga Tanzania Prisons na kesho anatarajia kukutana nao uso kwa uso kwenye mchezo wa kuhitimisha msimu huu 2022/23.

Mechi hiyo licha ya kuwa na umuhimu wa pande zote kumaliza kwa heshima, lakini ni muhimu zaidi kwa Mayele kutaka kufunga mabao ili kumaliza kinara na kutwaa tuzo ya mfungaji bora.

Hadi sasa nyota huyo amefunga mabao 16 akimuacha bao moja mpinzani wake Saido Ntibazonkiza anayecheza Simba na kufanya mechi za kesho kuwa za vita ya wawili hao.

Simba watafunga msimu kesho Ijumaa dhidi ya Coastal Union, ambapo viongozi na mashabiki wa timu hiyo pamoja na wachezaji kwa ujumla wakihitaji staa huyo raia wa Burundi aweze kuibuka kinara wa mabao ili kuwatoa kimasomaso baada ya kukosa mataji yote msimu huu.

Kocha Msaidizi wa Prisons, Shaban Mtupa amesema wamejipanga vyema kuendeleza ushindi kwani katika mechi tano za mwisho hajapoteza na hawatarajii kufungwa na Yanga mara mbili.

Amesema hata hivyo hawatapambana na mchezaji mmoja hususani Mayele badala yake watakomaa na timu nzima na kwamba rekodi yao hawajawahi kufungwa na Straika huyo.

"Hata Mayele hajawahi kutufunga na tunaenda kukutana naye ila tumejipanga kutopoteza mechi hiyo muhimu ili kuendeleza furaha kwa mashabiki wetu"

Nahodha wa timu hiyo, Jumanne Elfadhir amesema wachezaji wote wako fiti na matarajio yao ni kushinda mechi hiyo ili kumaliza ligi kwa heshima.

"Tuko tayari kwa mapambano na matarajio ni kushinda na mashabiki waje kwa wingi," amesema Elfadhir.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: