Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons: Kisasi ni haki

Wdqw Prisons: Kisasi ni haki

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

'Kisasi ni haki'. Ni kauli ya mashabiki wa Tanzania Prisons wakitambia timu yao kushinda mchezo wa leo dhidi ya Simba na kulipiza kisasi cha msimu uliopita.

Timu hizo zinatarajia kukutana saa chache zijazo katika mchezo wa Ligi Kuu, huku kumbukumbu ikiwa mbaya kwa Prisons waliofungwa nje ndani msimu uliopita.

Wakicheza nyumbani mechi ya kwanza walipoteza bao 1-0 huku wa marudio uwanja wa Taifa Dar es Salaam wakilala mabao 7-1.

Mchezo wa leo utakuwa aidha wa kuendeleza rekodi au kulipa kisasi kwa wapinzani hao ambao kila mmoja anahitaji pointi tatu kujiweka pazuri.

Katika mechi tatu zilizochezwa hadi sasa kwa timu hizo, Simba imeshinda zote na kuwa nafasi ya tatu kwa pointi tisa, huku Prisons wakiwa hawajashinda wakiambulia sare moja na kuwa mkiani kwa pointi moja.

Simba inahitaji kushinda mchezo huo ili kuchumpa kileleni kwa pointi 12 baada ya watani zao Yanga jana kupunguzwa kasi kwa kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu, huku Maafande hao wakitaka kujinasua mkiani.

Salim Issa shabiki wa Prisons amesema leo wanatarajia timu yao kufanya vizuri akiitabiria zaidi ya mabao mawili kutokana na ubora wa kikosi hicho.

"Tunaamini timu yetu ni bora na tunaenda kushinda zaidi ya mabao mawili, hatujapata ushindi hivyo tunaanza kazi leo nyumbani" amesema Issa.

Naye Isra Ngeli amesema kisasi ni haki na leo wanaenda kuwalaza Simba baada ya msimu uliopita kuwatesa akitambia uwezo na ubora wa wachezaji wa Prisons.

"Iliandikwa kuwa kisasi ni haki, msimu huu tunayo mabadiliko kikosini hivyo naamini tunaenda kupata pointi tatu" amesema Ngeli.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: