Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons, JKT Tanzania ni vita ya Maafande

Maafande JKT Prisons, JKT Tanzania ni vita ya Maafande

Sat, 21 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Tanzania Prisons na JKT Tanzania zikitarajia kushuka uwanjani kesho Jumapili Oktoba 22 katika mchezo wa Ligi Kuu, makocha na mastaa wa timu hizo wamerushiana tambo kila mmoja akisema ushindi upo.

Maafande hao wanakutana katika mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Sokoine jijini hapa ukiwa wa raundi ya sita, ambapo Prisons wapo nafasi ya 13 kwa pointi nne na JKT Tanzania wakiwa alama saba nafasi ya nane.

Timu hizo zinakutana ikiwa wenyeji wanajivunia rekodi ya kushinda mechi zote walizokutana katika michezo mitatu nyuma hivyo kufanya mpambano wa kesho kuwa wa visasi au kuendeleza ubabe.

Kocha mkuu wa Prisons, Fredi Felix 'Minziro' amesema ikiwa ni mchezo wao wa tatu nyumbani wanahitaji ushindi ili kuendeleza furaha kwa mashabiki.

"Tumeshapoteza mechi moja nyumbani na kushinda moja, hivyo kesho kazi itakuwa ni ushindi ili kuendeleza furaha kikosini na hata kwa mashabiki na kujinasua nafasi za chini," amesema Minziro.

Straika wa timu hiyo, Samson Mbangula amesema tangu mechi yao na Mtibwa Sugar morali imeendelea kuwa juu kwa wachezaji hivyo hata kesho matarajio yao ni kubaki na pointi tatu.

"Mbali na rekodi lazima twende kupambana kwa sababu hii ni mechi nyingine na wapinzani wamekuwa na matokeo mazuri ukilinganisha na sisi, hivyo kazi ya kocha imeisha kilichobaki ni kwetu," amesema Mbangula.

Kocha msaidizi wa JKT Tanzania, George Mketo amesema hawawezi kuingia uwanjani kwa matokeo ya zamani badala yake kesho ni mechi ya kutafuta pointi tatu na kwamba kikosi chake kipo fiti.

"Wale wanaoanza kikosi cha kwanza wote wapo sawa na hata hivyo hatuna mchezaji rasmi kila mechi isipokuwa kulingana na mchezo ndio tunaamua nani aanze au kusubiri ila kwa ujumla tuko tayari," amesema Mketo.

Naye straika wa timu hiyo, Hassan Kapalata amesema matokeo waliyoanza nayo kabla ya kupoteza mechi kadhaa nyuma, lakini kesho hesabu zao ni kuondoka na pointi tatu.

"Vijana wote tuko fiti na tunahitaji kuendeleza ushindi ukiachana na matokeo ya katikati ila tumeharejesha morali ya ushindi na kesho tunaamini ushindi upo," amesema Kapalata

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: