Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons: Hatuna mpango wa kumfukuza Minziro

Minzilro Msd Prisons: Hatuna mpango wa kumfukuza Minziro

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa klabu ya Tanzania Prison inayoshiriki ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara Jackson Mwafulango amesema kumekuwa na maneno mtaani kuwa timu hiyo ipo mbioni kuachana na kocha wake mkuu Fredy Felix Minziro ikiwa atapata matokeo mabovu mbele ya Simba.

Mwafulango amesema timu hiyo, haina mpango wowote kwa sasa wa kumundoa kocha huyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania.

Kocha Fredy Minziro hajawa na matokeo mazuri baada ya kukabidhiwa timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu baada kucheza mechi 3 pasipo na ushindi wa aina yoyote na kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya 16 katika ligi.

Mchezo unaofuata Tanzania Prison inatarajia kumenyana na Simba siku ya Tarehe 5 ya mwezi huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live