Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons, Geita Gold hakuna mbabe, makocha wakiri hali tete

Geita Vs Prisons.jpeg Prisons, Geita Gold hakuna mbabe, makocha wakiri hali tete

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Pamoja na kumaliza dakika 90 kwa suluhu ya bila kufungana, lakini makocha wa Geita Gold na Tanzania Prisons wamekiri hali haijawa sawa kikosini wakiahidi kurekebisha makosa ili kujiweka pazuri.

Katika mchezo wa leo ulipigwa uwanja wa Sokoine jijini hapa, licha ya timu zote kuonesha soka safi na la ushindani hakuna aliyeweza kuondoka na pointi tatu.

Matokeo hayo yanaifanya Prisons kukaa nafasi ya 12 kwa pointi saba, huku Geita Gold wakiwa nafasi ya 15 kwa alama sita baada ya timu zote kucheza michezo nane.

Kocha mkuu wa Geita Gold, Hemed Suleiman 'Morocco' amesema pamoja na matokeo hayo kuongeza morali kufuatia mechi iliyopita kufungwa 3-1 lakini bado kuna kukosa umakini kwa nyota wake.

Amesema mbali na kukosa umakini, lakini timu haijawa na muendelezo mzuri kama walivyoanza msimu akiahidi kukaa na mastaa wake kusahihisha makosa ili mechi ijayo nyumbani dhidi ya Tabora United kufanya kweli.

"Wanabadilika ila ni kidogo sana wanapoteza umakini hata kasi tuliyoanza nayo siyo ilivyo kwa sasa ila naamini tutarekebisha na timu itakaa pazuri, kimsingi ni vijana kupambana" amesema Morocco.

Kocha mkuu wa Prisons, Fredi Felix 'Minziro' amesema matokeo ya kutoruhusu bao si mabaya japokuwa straika wake hawakuwa makini kumalizia mipira ya mwisho akiahidi mechi zijazo watafanya vizuri.

"Tulihitaji pointi tatu na vijana walionesha uwezo lakini haikuwa bahati, beki walifanya kazi nzuri ila tulikosa umakini kufunga mabao tunashukuru kwa pointi moja" amesema Minziro.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: