Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prince Dube kwenye mtoko wa Pacome Day

Dube Kofia.jpeg Prince Dube kwenye mtoko wa Pacome Day

Sun, 25 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Azam FC ikiwa jijini Mbeya kupepetana na Tanzania Prisons, mshambuliaji wao Prince Dube yeye alikuwa Kwa Mkapa kwenye mtoko wa Pacome ili kushuhudia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na CR Belouizdad ya Algeria.

Yanga na Waalgeria walikipiga jana, huku mashabiki na baadhi ya wachezaji wakiwa wamehamasishwa kupaka blichi kichwani ili kulingana na mwenye siku yake, yaani Pacome Zouzoua na Dube ambae hayuko na kikosi hicho ikielezwa anasumbuliwa na majereha ni miongoni mwa mastaa mbali mbali waliotua katika mechi hii ya kimataifa.

Mshambuliaji huyo muhimu wa Azam, hii sio mara yake ya kwanza kufika katika mechi za Yanga licha ya kuwa na ushindani mkubwa katika ligi walionao.

Huenda akawa na mapenzi na soka ndio maana amehudhuria mechi hii ya hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.

Yanga ilishinda kwa kishindo mchezo huo kwa kuwafunga Belouizdad bao 4-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo kwa idadi kubwa ya mabao ya jead to head licha ya kwamba timu zote bado zina mchezo mmoja mkononi.

Kwa upande wao msimu huu Azam ilitolewa raundi ya kwanza na Bahir Dar Kanema ya Ethiopia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho ambako nako hawakufika mbali baada ya kutolewa mapema.

Rekodi zinaonyesha kuwa Dube ana jumla wa mabao saba huku kinara katika ligi akiwa na jumla ya mabao 10 akitokea Yanga, huku kinara wa kikosi hicho akiwa ni Feisal Salum mwenye mabao 8.

Katika Ligi nako Azam inashika nafasi ya pili ikiwa na jumla ya pointi 36 katika mechi 16 walizocheza na kesho itavaana na Prisons kwenye mechi ya Ligi Kuu itakapigwa Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live