Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prince Dube kuwakosa Pyramids

PRINCE Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube

Wed, 13 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Mshambuliaji hatari wa Klabu ya Azam Fc, Prince Dube atakosa mechi ya hatua ya pili ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri itakayochezwa Oktoba 16,2021 saa 9 alasiri katika uwanja wa Azam Complex.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na mawasiliano wa Azam Fc, Zacharia Thabit amesema Dube ndiye nyota pekee atakayekosekana katika mchezo huo  lakini wote waliosalia wapo katika hali nzuri.

Dube ambaye msimu uliopita alifunga bao 14 licha ya kucheza michezo michache kufuatia kuandamwa na majeraha, ameanza mazoezi mepesi baada ya kupatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata katika maandalizi ya msimu.

Vilevile Zaka Zakazi amesema kuwa wapinzani wapo, Klabu ya Pyramids inatarajiwa kuwasili nchini saa tatu usiku  na watafanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex.

Azam, Biashara na Simba ndizo klabu zilizosalia katika michuano ya kimataifa zikiiwakilisha Tanzania baada ya Yanga kutupwa nje mapema na Rivers United ya Nigeria.

Chanzo: eatv.tv