Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prince Dube aomba kuvunja mkataba Azam FC

Prince Dube Mpumelelo Prince Dube aomba kuvunja mkataba Azam FC

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC imethibitisha kupokea barua kutoka kwa mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube akiomba kuvunja mkataba na Klabu hiyo.

Ikumbukwe kuwa mkataba mpya wa nyota huyo raia hiyo aliyosaini mwaka 2023 ulipaswa kufikia ukingoni June 2026.

Azam FC imeweka bayana kuwa haina kipingamizi chochote na imemruhusu Dube kuondoka lakini matakwa ya kuvunja mkataba huo yafuatwe.

Akifafanua hilo, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria 'Zakazakazi' amesema;

“Azam FC inatuhibitisha kwamba tumepokea barua kutoka kwa Prince Dube, akiomba kuvunja mkataba na klabu yake ambayo ameitumikia tangu mwaka 2020. Dube amewasilisha barua kwa uongozi na uongozi umemjibu kama ifuatavyo;

“Kwanza mkataba wa Dube ambao alisaini mwishoni mwa msimu uliopita kabla ya kuanza kwa msimu huu unatakiwa kumuweka Azam FC hadi mwaka 2026, kwa hiyo hadi sasa bado ana miaka miwili na nusu.

“Klabu imemjibu kwamba jkama anataka kuondoa kama alivyowasilisha ombi lake haina kipingamizi hata kidogo, klabu inamruhusu kuondoka lakini mahitaji ya mkataba. Lazima mkataba utekelezwe kama mkataba wenyewe unavyotaka,” amesema Zakazakazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live