Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prince Dube: Natamani kucheza timu moja na na Aziz Ki, Chama

Chama Aziz Dube Prince Dube: Natamani kucheza na Aziz Ki na Chama

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mshambuliaji kinara wa Klabu ya Azam, Prince Dube amekiri kuwa anatamani kucheza timu moja na viungo washambuliaji Aziz KI wa Yanga na Clatous Chama wa Simba baada ya kukaa nje ya uwanja kwa nusu msimu sasa.

Dube amesema hayo wakati wa mchezo wa hisani 'Wape tabasamu' kati ya tema Kibwana Shomari na Team Dickson Job' uliopigwa juzi mjini Morogoro huku akifunga bao safi kati ya mabao 6 - 2 ambayo team Job walishinda.

Dube ambaye amevunja mkataba wake na Azama anatajwa kuibukia Yanga huku Chama naye ambaye mkataba wake umemalizika ndani ya yanga anatajwa kuibukia Yanga msimu ujao.

“Nimekuwa nikifanya mazoezi peke yangu lakini sijapata muda wa kucheza, nimemiss sana kuingia uwanjani na kucheza, nimemiss vibe la mashabiki kwa sababu watu wa Tanzania wanapenda soka na mashabiki wanawapenda wachezaji wao.

“Ni jambo kubwa kwangu na ninaamini kila mchezaji anatamani kucheza na wachezaji wakubwa hawa, kwa hiyo nikipata nafasi kama hiyo siwezi kuichukulia poa, kikubwa ni kuenjoy soka.

“Ofa zipo lakini nyingi sio Tanzania, ninaangalia itakayokuwa nzuri na tukakubaliana nitakwenda. Sitaki kuzungumzia kuhusu Simba ama Yanga. Mungu akipenda msimu ujao mashabiki watarajie kuniona tena uwanjani,” amesema Dube.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live