Wasudan wa Al Merrikh wameanza kuwa na wasiwasi juu ya Yanga kuelekea mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utachezwa Septemba 16.
Ni kawaida kwa Kocha yeyote kuwa ma tahadhari juu ya wachezaji hatari wa timu pinzani kabla hajakutana nao. Kwa sasa inaelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Al Merrikh Osama Nabieh ana wasiwasi na ubora wa Max Nzengeli na Zouzoua Pacome.
Kauli hii ya Kocha inafsiri katika mambo mawili,inawezekana kweli ana hofu na hao wachezaji ama anacheza na akili za benchi la ufundi la Yanga maana baadhi ya makocha wanajua kucheza mind game.
Kumbuka kwamba msimu uliopita wa 2022/2023 hatua kama hii Yanga walitolewa na Al Hilal SC ya Sudan ambayo inafundishwa na Kocha Florent Ibenge.