Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pre Season kwa timu za England 2024/25

Pre Season 2024 Pre Season kwa timu za England 2024/25

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati michuano ya Euro na Copa America ikiendelea kule Ujerumani na Marekani, timu mbalimbali barani Ulaya nazo zinajipanga kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya.

Baadhi ya timu hizo zinatarajiwa kubakia Ulaya, huku nyingine zikisafiri kwenda Asia na Marekani.

Hii hapa ratiba kamili ya timu sita kubwa za England juu ya wapi zitaenda kuweka kambi na mechi gani za kirafiki zitacheza katika kipindi cha kujiandaa na msimu mpya.

ARSENAL- MAREKANI

Baada ya kushindwa kuchukua taji la Ligi Kuu England katika dakika za mwisho msimu uliopita, Arsenal itasafiri kwenda Marekani kwa ajili ya kukusanya nguvu upya na kujiandaa na msimu ujao kuhakikisha inafanya vizuri.

Itakapokuwa nchini humo, itacheza mechi mbili tu za kirafiki ikianza na Manchester United Julai 27, kwenye uwanja wa SoFi Stadium uliopo Los Angeles, California, kisha itakutana na Liverpool Julai, 31, kwenye uwanja wa Lincoln Financial Field huko Philadelphia, Pennsylvania

CHELSEA - MAREKANI

Huu utakuwa ni msimu wa tatu kwa Chelsea kufanya maandalizi yake ya msimu nchini Marekani.

Mwaka jana maandalizi yake nchini humo yalimalizika kwa maumivu baada ya straika wao Christopher Nkunku kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund yaliyosababisha akae nje karibia msimu mzima.

Msimu huu itacheza mechi tano za kirafiki nchini humo ikianza kampeni hiyo dhidi ya Wrexham, Julai 24 kwenye Uwanja wa Levi’s Stadium, Santa Clara, California, kisha mechi nyingine ni dhidi ya-

vs Celtic -Julai 27 -Notre Dame Stadium, jijini, South Bend, Indiana

vs Club America - Julai 31 - Mercedes-Benz Stadium, jijini, Atlanta, Georgia.

vs Manchester City -August 03 -Ohio Stadium,jijini, Columbus, Ohio

vs Real Madrid - Agosti 06 - Bank of America Stadium, jijini, Charlotte, North Carolina.

LIVERPOOL - MAREKANI

Baada ya kuajiriwa akitokea Feyenoord wiki kadhaa zilizopita, Arne Slot atakuwa na kazi ya kusuka upya kikosi cha majogoo hao wa Jiji la Liverpool ili kupata mafanikio kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Jurgen Klopp.

Kambi yao ya maandalizi ya msimu itakuwa kule Marekani na nchezo wake wa kwanza kusimama katika benchi kama kocha wa Liverpool itakuwa ni dhidi ya Real Betis Julai 26, kwenye Uwanja wa Acrisure Stadium, Pittsburgh, Pennsylvania.

Baada ya hapo itaumana na Arsenal, Julai 31 kwenye dimba la Lincoln Financial Field, Philadelphia, Pennsylvania na mwisho itaumana na mashetani wekundu, Manchester United, Agosti 03 kwenye Uwanja wa Williams-Brice Stadium, Columbia, South Carolina.

MANCHESTER CITY - MAREKANI

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England ambao wamechukua taji hili mara sita katika misimu saba, wataanza kutesti mitambo kuanzia Julai 23 ambapo mechi zote zitapigwa kule Marekani ambako itajifua muda wote kabla ya kurejea England kuanza msimu mpya.

Man City itakutana na mabingwa wa Ligi Kuu Scotland, Celtic Julai 23, kwenye dimba la Kenan Stadium, Chapel Hill, North Carolina, kisha AC Milan, Julai 27 kwenye Uwanja wa Yankee Stadium, New York City.

Baada ya mechi hizo mbili itaenda kupiga mechi inayosubiriwa kwa hamu dhidi ya Barcelona ambapo Pep Guardiola ataenda kukutana na waajiri wake wa zamani, mechi hii itapigwa Julai 30, kwenye Uwanja wa Camping World Stadium, Orlando, Florida.

Mchezo wa mwisho itacheza dhidi ya Chelsea, Agosti 03 pale Ohio Stadium, Columbus, Ohio.

MANCHESTER UNITED - MAREKANI

Hii imekuwa ni kawaida sasa kwa mashetani wekundu hawa kujichimbia Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu na wamekuwa wakifanya hivyo kwa kile kinachoelezwa kwamba ni sababu za kibiashara.

Lakini kabla ya kwenda Marekani itakuwa na mechi mbili za kirafiki barani Ulaya, ya kwanza ni dhidi ya Rosenborg ya Norway Julai 15, ambapo itasafiri hadi nchini humo kucheza nao katika jiji la Trondhei, kisha itasafiri hadi Scotland kucheza na Rangers Julai 20, kwenye Uwanja wa Murrayfield.

Mechi nyingine:

vs Arsenal - Julai 27 - SoFi Stadium, jijini, Los Angeles, California

vs Real Betis - Julai 31 -jijini, Snapdragon Stadium, San Diego, California

vs Liverpool - Agosti 03 - jijini, Williams-Brice Stadium, Columbia, South Carolina.

TOTTENHAM - JAPAN, MAREKANI, SCOTLAND, KOREA KUSINI

Spurs ni kati ya timu zilizoanza maandalizi ya msimu mapema sana. Baada ya kumaliza msimu ilisafiri maili 10,500 kwenda Australia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Newcastle United Mei 22 na baada ya hapo imesafiri hadi Scotland, kisha itaenda Japan na Korea Kusini ambako itamaliza maandalizi yao ya msimu huo.

Licha ya kukosa wachezaji iliowahitaji huku staa wao Harry Kane akihama, Spurs bado ilianza vizuri Ligi Kuu England ikikusanya pointi 26 katika mechi 10 za mwanzo za ligi hiyo.

Baada ya Newcastle, mchezo mwingine wa kirafiki ambao itacheza ni dhidi ya Heart of Midlothian F.C. ya Scottland, Julai 17 kisha itavaana na QPR Julai 20 na baada ya hapo itasafiri hadi Japan kuumana na Vissel Kobbe, kisha itasafiri kwenda Korea itakakocheza na kikosi cha jumla cha Ligi Kuu nchini humo. Watamaliza na Bayern Munich huko Korea Agosti 03 na 10.

Chanzo: Mwanaspoti