Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Poulsen: Algeria ni timu kubwa, ni Taifa Kubwa, tunawaheshimu

Kim Paulsen Kim Paulsen

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen amesema Timu ya Taifa, Taifa Stars na nchi kwa ujumla lazima tuwaheshimu Algeria kwani ni timu kubwa na wanauzoefu mkubwa katika mashindano hayo hivyo ni wazi watakuwa na nafasi kubwa Zaidi yetu.

Poulsen amebanisha kuwa kwa ubora walionao Algeria ni wazi Tanzania inatakiwa kuingia uwanjani ikiwa na mpango maalum kwani akirejea namna ilivyocheza na Uganda kwa kiasi kikubwa Algeria ilikuwa na mpira muda mwingi kuliko Uganda.

Kocha huyo amesisitiza kuwa litakuwa ni jukumu la wachezaji kujitolea kufa kupona wapambane hadi tone lao la mwisho la damu, pia amesisitiza dhana ya kutumia uwanja wa nyumbani akisema kuwa ni kweli uwanja wa nyumbani una umuhimu sana na ni vema kuutumia vizuri lakini licha ya kuwa nyumbani haiondoi ukweli kwamba Algeria ni bora kuliko Tanzania.

Kwa upande mwingine Poulsen amewapongeza wachezaji wa akiba kwa ari wanayokuwa nayo licha ya kwamba wanakuwa nje ya uwanja lakini pia ameonesha kufurahishwa na namna ambavyo wachezaji wanaotokea benchi na kwenda uwanjani wanakwenda kubadilisha mchezo na kucheza kwa kuzingatia maelekzo yake.

Taifa Stars inawakaribisha Algeria kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa pili wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Ivory Coast.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live