Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Potter kupewa United huko

Graham Potter Kuwajibika Potter kupewa United huko

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Inaelezwa mkurugenzi mtarajiwa wa michezo wa Manchester United, Dan Ashworth amekutana na Kocha Graham Potter na maongezi yao yalihusu kuja kuchukua mikoba ya Erik ten Hag ambaye huenda akaondoka mwisho wa msimu.

Kumekuwa na wasiwasi juu ya hatma ya Ten Hag na kutokana na mwenendo wa timu hiyo na atafukuzwa mara moja kama itashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Hata hivyo, tajiri mpya wa miamba hiyo ya Old Trafford amekuwa akikataa kuongelea na kuweka wazi hatma ya kocha huyo iwapo ataendelea au atafunguliwa mlango wa kutokea, huku tetesi za Potter zikivuma tangu dirisha la usajili la majira ya kiangazi kwa sababu ana uhusiano wa karibu na tajiri huyo na kuna uwezekano mkubwa akatua mwisho wa msimu.

Potter hana kazi tangu aachane na Chelsea Aprili 2023 na haonekani kuwa kipenzi cha mashabiki wa Man United kutokana na rekodi zake akiwa na matajiri hao wa London.

Hata hivyo, inaelezwa Man United hadi inashindwa kukamilisha uhamisho wa Ashworth kutoka Newcastle kwani miamba hiyo ya St James Park imekuwa ikiweka ngumu kwenye pesa ya kuvunja mkataba wake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Mail, Man United inatakiwa kulipa kiasi kisichopungua Pauni 20 milioni kwa ajili ya kumsainisha na mazungumzo yapo kwenye hatua nzuri.

Inaelezwa tayari bosi huyo mpya ameshafikiana makubaliano na Man United na hiyo inaongeza uvumi wa kwa nini alikutana na Potter.

Chanzo: Mwanaspoti