Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Potter kiroho safi, atoa onyo kiaina

Potter Pic Graham Potter

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Chelsea, Graham Potter ameonya wakubali kupondwa na maneno ya watu kutokana na matumizi makubwa ya pesa waliyofanya kwenye dirisha dogo la usajili la Januari.

Potter akasisitiza maneno mengi yatazungumzwa hususan baada ya kuvunja rekodi ya usajili kitita cha Pauni 105 milioni walipomsajili kiungo wa kimataifa wa Argentina, Enzo Fernandez akitokea Benfica.

Licha ya usajili mkubwa uliofanywa na klabu hiyo Chelsea ikatoka suluhu bila ya kufungana ilipocheza dhidi ya Fulham wiki iliyopita.

Safu ya ushambuliaji ya Chelsea ilishindwa kupenya eneo la hatari kuambulia sare Mykhailo Mudryk akionyesha kiwango kibovu kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu England. winga huyo alisajiliwa kwa kitita cha Pauni 88 milioni, Benoit Badiashile aliyesajiliwa kwa kitita cha Pauni 35 milioni akianza kwenye mchezo.

Chelsea imeshindwa kupata ushindi katika mechi sita za mwisho walizocheza kwa mashindano yote msimu huu, vijana wa Potter wapo nafasi ya tisa ikiwa na pointi 30 baada ya sare dhidi ya Fulham.

Aidha Potter akajitetea akidai wanatakiwa kuimarika kiwango chao ili wapate matokeo mazuri kwenye ligi ligi kwasababu anaamini ana kikosi kipana.

"Tunatakiwa kuongeza bidii, ukiangalia siku za nyuma Chelsea ilikuwa haipat mabao, wakadhi kusajili mchezaji kwa Pauni 100 milioni ingesaidia tatizo, hili ndio tatizo kubwa, tuna changamoto kubwa sana, tunatakiwa tuwe makini," alisema Potter.

Mmiliki wa Chelsea,Todd Boehly alitumia kitita cha Pauni 300 milioni kwaajili ya usajili mwezi uliopita hata hivyo bado timu imeendelea kusuasua. Vile vile ikumbukwe Chelsea ilitumia Pauni 270 milioni kwenye usajili wa wachezaji wapya.

Chanzo: Mwanaspoti