Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Potter atanguliza jina la Rice mezani

Decline Rice Potter.jpeg Kiungo wa West Ham, Declan Rice

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa ulinzi wa West Ham United na England, Declan Rice, 23, ni miongoni mwa wachezaji ambao wamependekezwa na kocha mpya wa Chelsea, Gharam Potter kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Potter amependekeza jina la staa huyo ili akasaidiane na N’Golo Kante ambaye kwa miezi ya hivi karibuni amekuwa akipata majeraha ya mara kwa mara.

West Ham inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 90 milioni ili kumuuza fundi huyo.

Huyu anakuwa kocha wa pili kulilia huduma ya Rice baada ya Frank Lampard ambaye licha ya kuwasilisha jina lake, hadi anafukuzwa staa huyo hakusajiliwa.

Rice ni miongoni mwa mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha West Ham na msimu uliopita aliiwezesha timu hiyo kufika fainali ya Europa League.

Msimu huu West Hama haijaanza vyema ikipoteza mechi tano kati ya nane za kwanza kwenye Ligi Kuu na kushinda 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live