Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Potter atamba Chelsea

Potter Win Graham Potter

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Graham Potter amekiri ushindi waliopata wa bao 1-0 dhidi ya Leeds United ni mwanzo mzuri na anaamini timu yake itaendelea kupata matokeo mazuri katika mechi nyingine za ligi zinazofuata, baada ya kupoteza pointi nyingi msimu huu.

Chelsea ilipa ushindi wake wa pili katika mechi 12 za Ligi Kuu England walizocheza kabla ya kumenyana na Borussia Dortmund kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi Mabingwa Ulaya kesho. Mwezi uliopita mashabiki wa Chelsea walikuja juu na kuushinikiza uongozi wa Chelsea umtimue Potter kutokana na mwenendo mbovu wa timu, lakini kocha huyo akatuliza mzuka baada ya ushindi.

Aidha mmiliki wa klabu hiyo Todd Boehly akisisitiza anaamini Potter ni kocha mzuri na watampa muda akitengeneze kikosi chake baada ya usajili wa nguvu waliofanya.

Chelsea ilitumia kitita cha Pauni 323 kwenye dirisha dogo la usajili la Januari ilipowasajili Enzo Fernandez, Mykhailo Mudryk, Noni Madueke, Benoit Badiashile, David Fofana, Joao Felix alijiunga kwa mkopo, Andrey Santos na Malo Gusto, hata hivyo timu hiyo ilikuwa ikichezea kichapo.

Aidha Potter akadai ushindi dhidi ya Leeds umewapa nguvu kuelekea mchezo wao dhidi ya Dortmund utakaochezwa kesho uwanja wa Stamford Bridge.

"Nimefurahi baada ya ushindi huu, wachezaji wangu wameonyesha kitu, mashabiki walionyesha sapoti kubwa, tunafahamu mashabiki wanachotaka ni matokeo mazuri, kama timu ikifanya vibaya lawama zitapelekwa kwangu, kila mtu amefurahi na kujiamini, hii itasaidia zaidi kuelekea katika mechi zetu zinazofuata," alisema Potter.

Chelsea imejikita nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 34 baada ya ushindi waliopata dhidi ya Leeds.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live