Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Potter ashika mkia Chelsea

Graham Potter Kuwajibika Graham Potter

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Graham Potter ndiye kocha wa kwanza mwenye rekodi mbovu Chelsea tofauti na makocha wengine waliowahi kuinoa timu hiyo katika historia ya Ligi Kuu England.

Potter ameshinda michezo mitano tu katika michezo 18 na kufungwa michezo saba, hii ikizidi kumpa presha kocha huyo kwasababu timu bado haipati matokeo ya kuridhisha.

Katika michezo 15 ya mwisho ndani ya hizo mechi 18 ameshinda michezo miwili tu ya ligi mashabiki wakija juu wakishinikiza Potter afukuzwe kwasababu ameshindwa kazi iliyomleta.

Potter alipewa asilimia 27.8 hiyo ni mbovu zaidi tofauti na makocha wengine waliowahi kuinoa The Blues akiwemo Jose Mourinho, Avram Grant, Antonio Conte, Thomas Tuchel, Carlo Anceloti, Maurizio Sarri, Guus Hiddink, Roberto di Matteo, Caludio Ranieli na Frank Lampard, Potter akishika mkia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live