Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yatuma salamu Coastal Union

Polisi Tanzania Ft Polisi yatuma salamu Coastal Union

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Timu ya Polisi Tanzania, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbuni FC katika mchezo wao wa kirafiki uliopigwa katika viwanja vya ISM jijini Arusha, ikiwa ni maandalizi kuelekea michezo yao ya ligi.

Ushindi huo ni kama wametuma salamu za kujihakikishia kuvuna alama tatu dhidi ya wenyeji wao Coastal Union katika mchezo ujao wa mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Bao hilo pekee lililofungwa na mchezaji Idd Kipagwile dakika ya 84, lilitosha kumpa kiburi Kocha mkuu wa Polisi Tanzania, Joslin Bipfubusa aliyesema kuwa ushindani walioupata dhidi ya Mbuni ya Daraja la Kwanza, umetosha kuona uimara wa kikosi chake.

"Kwanza tumefurahi kucheza na timu hii ya daraja la kwanza lakini zaidi tumeona wako vizuri na wametupa Ushindani mkubwa kwa jinsi walivyojiandaa, lakini zaidi nimeona kikosi changu kimeimarika tofauti na michezo miwili ya awali ya kufungua ligi dhidi ya Yanga na KMC"

Alisema kuwa maandalizi makubwa yanaendelea katika kikosi chake kuelekea mchezo wa Coastal Union ya Tanga na anaamini atafanikiwa kuvuna alama tatu.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Polisi Tanzania, Robert Munis alisema kuwa wanakwenda kuvunja uteja dhidi ya Coastal Union baada ya kufungwa mechi zote msimu ujao za nyumbani na ugenini.

"Huo mchezo tunataka kuonyesha wapinzani wetu kuwa sisi sio wanyonge wao bali walituotea tu msimu uliopita hivyo niwaahidi mashabiki na wapenzi wa Polisi Tanzania wategemee furaha ya point tatu dhidi ya Coastal Union hapa Sheikh Amri Abeid Arusha"

Kocha wa timu ya Mbuni, Leonard Budeba alisema kuwa wamefurahi kupata mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania kwani imekuwa kipimo kizuri kwao kujua hali ya kikosi.

"Huu mchezo umetufunza mengi ikiwemo mapungufu madogo madogo yaliyoko kwenye kikosi hivyo nakwenda kuyafanyia kazi kuhakikisha naimarisha kikosi zaidi na kuchagua kikosi cha kwanza mapema ili kuhakikisha nafanya vizuri kwenye ligi daraja la kwanza".

Nae mwenyekiti wa timu ya Mbuni, Felician Mashauri alisema kuwa mwaka huu timu hiyo wamejipanga vema kuhakikisha wanafanya vizuri katika Mashindano hayo Ili kuipa nafasi Arusha kuwa na timu ya ligi kuu.

"Ligi daraja la kwanza ni ngumu sana na tunajua maana nilikuwa nafuatilia hata kabla hatujapanda, hivyo na sisi tumejiandaa kikabiliana nazo, hivyo nitumie nafasi hii kuwaomba wadau watupe sapoti hasa ya kiuchumi malengo haya yatimie haraka "

Chanzo: Mwanaspoti