Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yamtolea macho Dilunga

94369 Dilunga+pic Polisi yamtolea macho Dilunga

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Polisi Tanzania inatakiwa kuwa makini leo na wachezaji wa viungo wa Simba ambao wameonekana kuwa na kasi ya kufunga mabao katika mechi za hivi karibuni.

Simba itaikaribisha Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam huku ikijivunia viungo hodari wakiongozwa na Hassan Dilunga ambaye amekuwa katika kiwango bora.

Safu ya ulinzi ya Polisi Tanzania chini ya kipa Mohammed Yussuph na mabeki William Lucian,Yassin Mustapha, Mohammed Kassim, Idd Mobby na Pato Ngonyani wanatakiwa kumpa ulinzi Dilunga.

Dilunga ameonekana kucheza kwa kiwango bora katika michezo mitano iliyopita ya hivi karibuni iwe ameanza kikosi cha kwanza au akitokea benchi, hivyo kuwa mmoja wa wachezaji hatari katika kikosi cha Simba.

Kiungo huyo wa zamani wa Yanga na Ruvu Shooting amefunga mabao matatu katika mechi tano za Simba akitoa pasi mbili za mabao.

Si Dilunga pekee kwani hali ya kupambana kwa viungo wa Simba ndani ya kikosi chao imeonekana kuongezeka maradufu hivyo kuipa matokeo muhimu timu hiyo katika mechi za ligi.

Pia Soma

Advertisement
Katika mchezo dhidi ya Mbao ambao Simba ilishinda mabao 2-1 yaliyofungwa na Dilunga, Jonas Mkude ambaye ni kiungo.

Mchezo dhidi ya Alliance ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 4-1, yalifungwa na Mkude, Dilunga, Clatous Chama na Meddie Kagere.

Katika mchezo ambao Simba iliichapa Namungo mabao 3-2 yalifungwa na Dilunga, Kahata, Kagere. Dhidi ya Coastal Union mabao ya kiungo Mbrazili Gerson Fraga ndiyo yaliyoipa ushindi wa mabao 2-0 Simba.

Wakati Simba ikitambia rekodi ya wachezaji wa kiungo, kocha msaidizi wa Polisi Tanzania, Ally Mtui alisema licha ya kucheza mechi hiyo ndani ya muda mfupi, wamejipanga kushinda.

Polisi Tanzania juzi ilimaliza mchezo wake dhidi ya JKT Tanzania baada ya mvua kukatisha mechi hiyo Jumamosi. Timu hiyo ilishinda bao 1-0.

Kiungo wa zamani wa Yanga Pato Ngonyani alisema ni mechi muhimu kwa upande wao na wanataka kupata matokeo mazuri licha ya kutambua ubora wa wapinzani wao ambao wanaongoza Ligi Kuu kwa pointi 47.

Chanzo: mwananchi.co.tz