Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamdaka Rashid Juma

Rashid+juma+pic Polisi wamdaka Rashid Juma

Thu, 27 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Yohana ChalleWinga wa Simba, Rashid Juma ametua kwenye kikosi cha Polisi Tanzania kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Juma ameondoka kwenye kikosi cha Simba kutokana na ushindani wa namba baada ya usajili unaofanywa na mabosi wa timu hiyo na kujikuta akiishia benchi.

Wachezaji wengine waliotambulishwa hadi sasa ndani ya Polisi Tanzania ni pamoja na Daruweshi Saliboko aliyekuwa akikitumikia kikosi cha Lipuli FC msimu uliopita na kufunga mabao 11 kwenye Ligi Kuu.

Tetesi za awali zilieleza mchezaji huyo angeweza kujiunga na KMC lakini ushawishi wa Polisi Tanzania ukamfanya abadili gia angani.

Mchezaji mwingine ni kinda Kassim Shaban Haruna 'Tiote' amejiunga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Sahare All Stars ambayo msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Pili (SDL).

Datus Peter ambaye amejiunga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mbao FC kama ilivyo kwa Ramadhan Kapera ambaye ni mchezaji huru na msimu uliopita alikuwa KMC.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz