Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wafuta wafuta mchezo wa Arsenal, PSV Europa

Emirates uwanjani Emirates

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mechi ya makundi ya Europa League baina ya Arsenal na PSV imefutwa kutokana na upungufu wa polisi wa kulinda usalama kufuatia maziko ya Malkia Elizabeth II.

Mechi za Ligi Kuu England, EFL, WSL na mechi nyingine za timu za watoto zilifutwa wikiendi iliyopita baada ya tangazo la kifo cha Malkia Elizabeth II, 96 kilichotokea Alhamisi iliyopita. Mechi ya usiku wa Jumatatu pia iliyokuwa ikizikutanisha Leeds United na Nottingham Forest nayo iliahirishwa.

PSV sasa imethibitishwa kwamba mechi yao dhidi ya Arsenal iliyopangwa kufanyika Alhamisi uwanjani Emirates imeahirishwa.

Hiyo ni kwasababu ya hofu ya kutokea kwa uchache wa polisi huko London kwa kipindi hicho cha mechi kufanyika kwa sababu watakuwa kwenye majukumu ya msiba.

Taarifa iliyotolewa na PSV ilisomeka: "Taarifa iliyotolewa na mamlaka ya Uingereza kunaweza kutokea upungufu wa polisi kutokana na shughuli za maziko ya Malkia Elizabeth zitakazofanyika London."

Chelsea watacheza mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya siku wa Jumatano dhidi ya RB Salzburg na mechi hiyo itafanyika. Ishu ya polisi haihusiani na shughuli zitakazofanyika nje ya London.

Liverpool wao watakuwa na mechi dhidi ya Ajax uwanjani Anfield na Manchester City watakipiga na Borussia Dortmund huko Etihad na mechi zote hizo zitafanyika kama zilivyopangwa. Tottenham, West Ham na Manchester United nazo zitacheza ugenini, hivyo mechi zao zitaendelea kama kawaida.

Hata hivyo, mechi za wikiendi ijayo kwenye Ligi Kuu Englana zipo kwenye hatihati ya kuahirishwa kutokana na sababu za kiusalama.

Maziko ya Malkia Elizabeth II yatafanyika Jumatatu, Septemba 19 na kuna mechi mbili za kibabe za ndani ya jiji la London wikiendi ijayo. Brentford watacheza na Arsenal na Chelsea watakipiga na Liverpool uwanjani Stamford Bridge. Bado haifahamiki kama mechi hizo zitafanyika licha ya kipute cha Stamford Bridge kuwa na dalili zote za kuahirishwa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz