Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tz mbele ya Dodoma Jiji ni kufa au kupona

Polisi Tanzania Hali Tete.jpeg Kikosi cha Polisi Tanzania

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Tanzania imejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, huku ikitamba haitashuka daraja.

Timu hiyo inaburuza mkia ikiwa na pointi 19 katika michezo 24 iliyocheza mpaka sasa na mchezo wa mwisho dhidi ya Mbeya City ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Polisi Tanzania katika michezo 24, iliyocheza mpaka sasa inashika nafasi ya tatu kwa kufungwa mabao mengi 33,huku Mtibwa Sugar na Mbeya City zikifungwa mabao 35.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 11,2023 Jijini hapa kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Dodoma Jiji,unaotarajiwa kufanyika saa 2 usiku, kocha msaidizi wa timu hiyo, Mohammed Silima amesema wanaamini utakuwa mchezo mgumu lakini wamejipanga kushinda.

Amesema wanaendelea kushughulikia tatizo la ufungaji kutokana na timu hiyo kufunga mabao 18 pekee katika michezo 24 iliyocheza mpaka sasa.

“Ni kweli tumefunga mabao machache tulikuwa na tatizo la washambuliaji wetu kuwa majeruhi sasa hivi wamepona na wapo vizuri,”amesema kocha huyo. Amesema Dodoma Jiji isitarajie mteremko katika mchezo huo kwani wameisoma na kujua udhaifu wao na ubora wao upo wapi.

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo,Tariq Simba amesema anafurahi kurudi kucheza katika ardhi aliyozaliwa huku akiahidi watacheza kwa kupambana kuhakikisha wanapata matokeo.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo,Kassim Liogope amesema wAmesema ataendelea kukosa huduma ya wachezaji Stephen Sey na Chriastin Zigar kutokana na kuumia.

“Kuhusu Randy Bangala yule ni mchezaji wetu mwanzo alikuwa na changamoto ya vibali lakini katika mzunguko wa pili vimepatikana na alikuwa katika sehemu ya kikosi chetu kilichoenda Dar es salaam akiwa sawa atacheza tu,

Chanzo: www.tanzaniaweb.live