Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tz, Simba shilingi imesimama

Moses Phiri Goals.jpeg Mshambuliaji wa Simba, Moses Phiri

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafande wa Polisi Tanzania wanashuka kwa mara ya kwanza katika uwanja wao wa nyumbani wa Ushirika mjini Moshi kumenyana na Simba baada ya kufanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo sehemu ya kuchezea ambayo ilifanya ifungiwe na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Mchezo huo utapigwa leo Jumapili ambapo utaanza kutimvua vumbi kuanzia majira ya saa 10:00 za jioni huku ukitazamiwa kuwa mgumu kutokana na matokeo ambayo timu hizo zimepata katika mechi zilizopita.

Polisi ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro huku Simba ikilazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Simba inaihitaji pointi zote tatu ili kupunguza gepu dhidi ya vinara Yanga wenye 32 baada ya michezo 12 pamoja na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa alama 29 baada ya michezo 13 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 28 baada ya michezo 13.

Maafande wa Polisi Tanzania nao hawajapata matokeo ya kuridhisha katika mechi zake za nyumbani iliyocheza kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha na Black Rhino Karatu lakini pia katika viwanja vya ugenini inahitaji kushinda ili kurudisha morali kwa mashabiki lakini pia kujitengenezea mazingira ya kutoka nafasi za chini.

Timu hiyo inashika nafasi ya 14 katika msimamo kwa pointi tisa pekee baada ya michezo 13 ,imeshinda mechi mbili, sare tatu na kupoteza nane huku ikiwa imefunga mabao 10 na kufungwa 19.

Hata hivyo rekodi haimbebi Polisi dhidi ya Simba kwani katika michezo sita ambazo wamekutana tangu timu hiyo ilipopanda Ligi Kuu msimu wa 2019/20 na kuanza imeambulia sare moja na kupoteza tano.

Kwa mara hizo sita ambazo wamekutana Simba imevuna pointi 15 na mabao nane huku Polisi Tanzania ikipata pointi moja pekee na mabao mawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live