Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tz, Coastal Union mechi ya magoli Ushirika Moshi

CADF56DE 3217 4AA5 8425 488914DDE1DB.jpeg Kikosi cha Polisi Tanzania

Tue, 27 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Polisi Tanzania wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mabao ya Polisi Tanzania yamefungwa na Ally Rutibinga dakika ya 10 na Kelvin Sabato dakika ya 41 na 80, wakati ya Coastal Union yamefungwa na Vincent Abubakar dakika ya 18, Chilo Mkama aliyejifunga dakika ya 48 na Gustapha Simon dakika ya 89.

Kwa matokeo hayo kila timu ikicheza mechi ya 18 ya msimu, Polisi Tanzania wanafikisha pointi 10, ingawa wanaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 wakizidiwa pointi tano na Coastal Union inayobaki nafasi ya 14.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live