Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania yasaini dili Dodoma

POLISI TZ.png Polisi Tanzania yasaini dili Dodoma

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: dar24.com

Timu ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC leo imeingia mkataba wa Udhamini wa Maji ya kunywa na Nabii Clear Malisa wa Kanisa la Heaven Of Peace Kingdom Embassy.

Maji hayo aina ya Jordan yatatumika kwa ajili ya Kambi , mazoezini, michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, Safarini na Vikao vyote vya timu hiyo.

Mkataba huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 50 umesainiwa leo Jumanne (Oktoba 04) Jijini Dodoma, kati ya Nabii Malisa na Katibu Mkuu wa Timu hiyo ASP Michael Mtebene.

Aidha, udhamini huo umejikita katika kuboresha mitandao ya kijamii ya timu kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano.

Chanzo: dar24.com