Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania yafichua siri ya kuongoza Ligi

POLISI TANZANIA Vinara wa Ligi kuu Bara

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo kwa sasa inatambulika kama Ligi kuu ya NBC, imesimama kwa muda kupisha kalenda ya FIFA.

Mpaka ilipofikia hatua kusimama, tayari kila timu imekwishacheza michezo miwili, na timu ya Polisi Tanzania kutoka kule Moshi Mkoani Kilimamnjaro ndiyo inayoongoza Ligi ikiwa na alama 6.

Robert Munisi , Makamu mwenyekiti wa Polisi Tanzania amesema siri kubwa ya wao kuongoza ligi mpka sasa ni kutokana na kuwepo kwa uongozi bora, benchi la ufundi bora na mashabiki bora.

Wakati wanajiandaa kwa mchezo wao na Simba Oktoba 20, Munisi amesema misimu iliyopita walipoteza mechi zao zote dhidi ya mnyama lakini safari hii wanachotamani ni kucheza na Simba.

Munisi amefafanua kuwa wanawaheshimu Simba kwa ubora na ukubwa wao lakini kamwe hawawaogopi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live