Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania yaendelea ilipoishia

POLISI TZ.jpeg Polisi Tanzania waibuka na ushindi ugenini

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Tanzania ni kama hawakamatiki na wanaendelea pale walipoishia kabla ya mechi yao dhidi ya Simba SC ambayo ilikuwa ipigwe Oktoba 20,kusogezwa mbele

Bao pekee la mshambuliaji Vitalis Mayanga dakika ya 78, limeipa Polisi Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Uwanja Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Ushindi huo unaifanya Polisi ifikishe pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu na sasa inalingana kila kitu na vigogo, Yanga SC wanaoongoza Ligi, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake sita za mechi nne sasa katika nafasi ya nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live